NIGERIA

Boko Haramu yaendelea na visa vya utekaji nyara Nigeria

Kibao cha shule ya wanafunzi wa kiume waliotekwa na kundi la Boko Haram
Kibao cha shule ya wanafunzi wa kiume waliotekwa na kundi la Boko Haram Daily Trust

Kundi la kigaidi la Boko Haram nchini Nigeria limesema lilihusika na utekaji nyara wa wanafunzi wa shule ya Wavulana zaidi ya 300 katika jimbo la Katsina, Kaskazini Magjharibi mwa nchi hiyo Ijumaa iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau kupitia mkanda wa video amesema wapiganaji wake walichukua hatua hiyo kwa sababu elimu wanayopata wavulana wa shule hiyo ya Kankara ni kinyume na mafundisho ya Kiislamu.

Katika hatua nyingine, Gavana wa jimbo la Katsina Aminu Bello Masari baada ya kukutana na rais Muhamadu Buhari, amesema kuna matumaini ya kuwaokoa wanafunzi hao.

Mwaka 2014 kundi hilo la Boko Haram liliwateka wasichana 276 wa shule ya Sekondari ya Chibok, katika Jimbo la Borno.

Shinikizo zimeendelea kutolewa kwa serikali nchini humo kuwaokoa wanafunzi hao.