ETHIOPIA

Mapigano kati ya wanajeshi wa Ethiopia na Sudan katika eneo la el-Fashaga

Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed
Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed © Tiksa Negeri / REUTERS

Jeshi la Sudan limesema lilivamiwa na vikosi vya jeshi la Ethiopia katika eneo la mpaka, na kusababisha mzozo kati ya nchi hizo mbili.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kwa vyombo vya habari jeshi hilo la Sudan linaonyesha kwamba limepata hasara kubwa katika mapigano hayo, likisema kuwa limepoteza wanajeshi kadhaa na vifaa kadhaa kuharibiwa.

 

Mapigano hayo yalitokea wakati kikosi cha wanajeshi wa Sudan waliokuwa wakipiga doria walipokuwa njiani wakirudi karibu na eneo la Jebel Abutiour, huko el-Fashaga, Kusini Mashariki mwa mji wa Gedaref.

 

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatano jioni, Abdallah Hamdok hakutoa maelezo zaidi kuhusu mapigano hayo, lakini alibaini, askari wake 'walikumbwa na shambulizi la kushtukiza' lililotekelezwa na "vikosi vya Ethiopia na wanamgambo". Amevitaka vikosi vya jeshi 'kulinda mipaka ya nchi na kurudisha nyuma uvamizi wowote'.