DRC

Masharti mapya ya kupambana na Covid 19 yatangazwa nchini DRC

Felix Tshisekedi rais wa DRC
Felix Tshisekedi rais wa DRC REUTERS/Hereward Holland

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mlipuko wa pili wa maambukizi ya Covid 19 umetangazwa siku chache zilizopita, hatua ambayo imempelekea rais Felix Tshisekedi kutangaza masharti mapya ikiwa ni pamoja na kuwazuia watu kutembea kote nchini humo kati ya saa tatu usiku mpaka saa kumi na moja Alfajiri kuanzia siku ya Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya COVID 19 katika nchi hiyo ambayo imeshuhudia visa  vipya 345 likiwemo jiji la Kinshasa ambalo lilikuwa na visa 298, huku watu sita wakipoteza maishga siku ya Jumanne, kwa mujibu wa Wizara ya afya.

Taarifa ya rais kuhusu masharti mapya imeeleza kuwa maambukizi yameongezeka kutokana na wageni wanaowasili nchini humo ambao wameambukizwa.

Kote nchini humo watu hawataruhusiwa kutembea kati ya saa tatu usiku hadi saa 11 Alfajiri na sherehe ya sikukuu pamoja na  mikutano ya zaidi ya watu 10 imezuiwa.

Wanafunzi wa Shule za msingi ,na sekondari wataanza likizo ya mapema kuanzia siku ya Ijumaa, lakini haijafahamlika ni lini watarudi Shuleni huku wanafunzi wa  elimu ya juu masomo yao yakiahirihswa.

Maandamano yamezuiwa pia, huku michezo ikiendelea bila ya mashabiki lakini mazishi yataendelea bila ya shetrehe zozote.

Maeneo ya kuabudu na burudani yataendelea kama kawaida chini ya mashrti ya Wizara ya afya lakini sio wakati wa watu kutotembea.

Tarehe 24 Machi  hali ya dharyra ilitanagzwa katilka maeneo kadhaa nchini hiumo ikiwemo jiji kuu Kinshasa lakini ikaondolewa Julai 22.