DRC

COVID-19 DRC: Hali ya wasiwasi yatanda kabla ya kuanza kutekelezwa masharti mapya

Rais wa DRC, Félix Tshisékédi.
Rais wa DRC, Félix Tshisékédi. Tchandrou Nitanga / AFP

Wakati Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inaendelea na kukabiliwa na mlipuko wa pili wa ugonjwa hatari wa COVID-19, nchi hiyo inatarajia kuanza kutekeleza sheria ya kutotembea leo Ijumaa jioni, Desemba 18.

Matangazo ya kibiashara

Sheria hiyo itaanza saa 3 usiku hadi saa 11 alfajiri. Kutembea wakati wa kipindi chote cha amri ya kutotoka nje itatokana na kibali maalum kutoka kwa mamlaka ya mkoa, isipokuwa kwa watu walio katika hali za dharura kiafya.

 

Uamuzi huu utaathiri Wakongo wengi na wengi wana wasiwasi kuhusu sheria hiyo.

 

Hatua hii imekuja kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya COVID 19 katika nchi hiyo ambayo imeshuhudia visa  vipya 345 likiwemo jiji la Kinshasa ambalo lilikuwa na visa 298, huku watu sita wakipoteza maisha siku ya Jumanne, kwa mujibu wa Wizara ya afya.

 

 Taarifa ya rais kuhusu masharti mapya imeeleza kuwa maambukizi yameongezeka kutokana na wageni wanaowasili nchini humo ambao wameambukizwa.

 

 Kote nchini humo watu hawataruhusiwa kutembea kati ya saa tatu usiku hadi saa 11 Alfajiri na sherehe ya sikukuu pamoja na  mikutano ya zaidi ya watu 10 imezuiwa.