NIGERIA

Wanafunzi waliotekwa Nigeria, waachiliwa

Nigeria: Picha iliyochukuliwa kutoka kwenye mtandao wa kijamii wa facebook ukiwaonesha wanafunzi wanaodaiwa walitekwa
Nigeria: Picha iliyochukuliwa kutoka kwenye mtandao wa kijamii wa facebook ukiwaonesha wanafunzi wanaodaiwa walitekwa Facebook/screenshot

Gavana wa jimbo la Kasina, kaskazini mwa nchi ya Nigeria, amethibitisha kuachiwa kwa mamia ya wanafunzi wa kiume waliotekwa juma lililopita na wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram.

Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha jimbo la Katsina, NTA, gavana wa jimbo la Katsina, Aminu Bello, amesema wavulana wapatao 344 wameokolewa na maafisa wa usalama, wakati wakisubiri kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabau kabla ya kuruhusiwa kujumuika na familia zao.

Hata hivyo haijabainika wazi idadi kamili ya wavulana ambao wangali mikokoni mwa watejaki wao, baada ya kundi la Boko harama kusambaza video iliomuonesha mvulana mmoja akisema ni miongoni mwa wanafunzi 520 waliotekwa nyara.

Rais Muhammadu Buhari kupitia ukurasa wake wa Twitter, ametaja hatua hiyo kama ya kuleta utulivu katika taifa nzima na hata jamii ya kimataifa, rais Buhari akitoa wito wa uvumilivu wakati serikali yake ikijitahidi kukabiliana na utovu wa usalama.

Tukio hili la ijumaa iliopita limezua wasiwasi juu ya hali ya utovu wa usalama na machafuko unaoendelea kushiuhudiwa  kaskazini mwa nchi hiyo.

Kuachiwa kwao kumekuja saa chache tu tangu kundi la Boko Haram, litoe picha za video zikiwaonesha iliyodai baadhi ya wanafunzi ambao ilikuwa imewateka juma lililopita.

Hata hivyo mamlaka nchini Nigeria, hazijaweka wazi idadi kamili ya wanafunzi ambao hadi sasa bado hawajapatikana.