JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

CAR: Mvutano waibuka siku chache kabla ya uchaguzi

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Toudéra.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Toudéra. Ludovic MARIN / AFP

Hali ya usalama imeendelea kuzorota nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu Ijumaa, Desemba 18, siku tisa kabla ya Uchaguzi Mkuu nchini humo. Miji kadhaa magharibi mwa nchi imeshambuliwa na wapiganaji wa makundi mbalimbali yenye silaha, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Matangazo ya kibiashara

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA, imetuma wanajeshi wake wengi katika miji hiyo na kusema iko katika "tahadhari kubwa" katika mikoa mingine, pamoja na mji mkuu, Bangui.

Tume hiyo ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) imelaani mfululizo wa 'mashambulizi yaliyoratibiwa' yenye lengo la "kuzuia" uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba 27.

Kulingana na vyanzo vinavyoaminika, maeneo kadhaa magharibi mwa nchi yalivamiwa siku ya Ijumaa na watu wenye silaha.

Umoja wa Mataifa unasema umepeleka vikosi vyake kaika miji ya  Bossemptele na Bossembele, kilomita 150 kaskazini magharibi mwa Bangui, na unasema miji ya Bozoum na Yaloke pia imeshambuliwa.

Umoja wa Mataifa umeyahusisha makundi ya matatu yenye silaha ya 3R, MPC na anti-balaka na mashambulizi haya.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, askari wa wawili wa vikosi vya serikali wameuawa katika shambulio la Yaloke.

Fatou Bensouda, mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, amehakikisha kuwa hali hiyo inafuatiliwa kwa karibu.

Mvutano umeongezeka baada ya François Bozizé kukataliwa kuwania katika uchaguzi wa urais na pia kukutana na makundi yenye silaha