ETHIOPIA

Ethiopia: Mapigano yaendelea Tigray

Wanajeshi wa Ethiopia wanaopambana katika jimbo la Tigray
Wanajeshi wa Ethiopia wanaopambana katika jimbo la Tigray REUTERS/Tiksa Negeri/File Photo

Nchini Ethiopia, mapigano yanaendelea kushuhudiwa katika jimbo la Tigray, lakini imekuwa ni vigumu kufahamu ni wapi yanapotokea kwa sababu ya mawasiliano mabaya. 

Matangazo ya kibiashara

Zimepita siku 45 tangu Waziri Mkuu Abiy Ahmed aagize operesheni ambayo ilibaini kuwa imemalizika ingawa hakuna kiongozi hata mmoja wa chama cha Tigrayan TPLF ambaye amekamatwa.

Ahmed ameendelea kutegemea kupata uugwaji mkono kutoka kwa  vikosi vya Eritrea, hata kama Asmara inaendelea kukanusha kuhusika katika vita hivyo.

Aidha, anaendelea kupata  msaada mkubwa kutoka kwa wanamgambo na vikosi maalum katika mkoa wa Amhara, ambao unapakana na Tigray.

Wapiganaji wa Amhara, jamii ya pili kwa ukubwa nchini Ethiopia, wamedhibiti maeneo yanayodai kuwa ya vikoi vya TPLF.

Mzozo huo ambao bado haujamalizika huko Tigray kwani maafisa katika mkoa wa Amhara tayari wanataka kutekeleza shambulio kama hilo katika jimbo jirani la Benishangul Gumuz.

Jimbo hili tata la kikabila la watu milioni moja ndio eneo la mapigano ya kikabila ambayo yamesababisha vifo vya watu wengi na maelfu kuyatoroka makazi yao katika miezi ya hivi karibuni.