MALI

Serikali ya Mali yafunguliwa mashtaka kuhusu ukeketaji

Moja ya kifaa ambacho hutumika wakati wa ukeketaji
Moja ya kifaa ambacho hutumika wakati wa ukeketaji UN

Siku chache zilizopita Mashirika manne yanayotetea haki za wanawake yaliwasilisha malalamiko yao dhidi ya serikali ya Mali kufumbia macho kitendo cha ukeketaji katika mahakama ya ECOWAS huko Abuja, nchini Nigeria.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya asilimia 80 ya wanawake wa Mali ni waathirika wa ukeketaji, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

 

Shirika la Afya Diunia, WHO, linasema sio tu kwamba ukeketaji ni ukiukaji wa haki za binadamu lakini unaathiri afya kimwili na kiakili kwa mamilioni ya wasichana na wanawake na pia kutumia raslimali nyingi muhimu za nchi na kwamba uwekezaji zaidi unahitajika kumaliza ukeketaji na madhila unaosababisha.

 

Kwa mujibu wa makadirio mapya gharama ya matibabu kutokana na athari za ukeketaji huenda ikafika dola bilioni 1.4 kimataifa kwa mwaka iwapo mahitaji yote ya kiafya yatashughulikiwa. Katika nchi binafsi, gharama hii inakaribia asilimia 10 ya matumizi ya mwaka mzima ya afya kwa wastani ambapo katika baadhi ya nchi idadi hii huenda ikafika asilimia 30.

 

WHO inasema wanawake na wasichana waathirika wa ukeketaji wanakabiliwa na hatari kubwa katika afya yao na uzima, hii ni pamoja na athari pindi tu baada ya kukeketwa ikiwemo: maambukizi, kuvuja damu nyingi au kiwewe pamoja na magonjwa ya muda mrefu ambayo huenda yakatokea maishani.

 

Pia wanawake ambao wamekeketwa wana uwezekano mkubwa wa kupata tishio la kupoteza maisha wakati wa kujifungua, kukabiliwa na magonjwa ya akili na maambukizi ya muda mrefu.

 

Pia huenda wakahisi uchungu wakati wa hedhi, wakienda haja ndogo au wakati wa kitendo cha kujamiana, WHO imebaini.