SUDAN-ETHIOPIA

Viongozi wa Sudan, Ethiopia kujadiliana kuhusu mzozo wa mipaka

Waziri mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdock.
Waziri mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdock. ASHRAF SHAZLY / AFP

Majadiliano kati ya Sudan na Ethiopia kuhusu mgogoro kwenye maeneo yao ya mipaka, yatafanyika Jumanne ya wiki ijayo, ikiwa ni wiki moja tangu vikosi vya nchi hizo mbili vipigane.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu wa Sudan, Abdalah Hamdock, kiongozi huyo atakutana na mwenzake wa Ethiopia, Abiy Ahmed, kujadiliana kuhusu uundwaji wa kamati maalumu itakayoshughulikia suala hilo.

Mkutano wa viongozi hawa wawili unafanyika kando na mkutano wa wakuu wa nchi za IGAD, unaofanyika nchini Djibouti.

Mkutano wa mwisho kuhusu mzozo wa maeneo ya mpaka baian ya nchi hizi mbili ulifanyika mwezi Mei mwaka huu jijini Addis Ababa.

Msimu wa mvua ni miongoni mwa mambo ambayo yalikwamisha kamati za nchi zote mbili kukutana.

Mpaka wa awali ulichorwa na Uingereza wakati wa ukoloni, ambapo uliacha maeneo kadhaa ya mpaka baina ya nchi hizo mbili kwenye utata mkubwa, hali ambayo mara kadhaa imeshuhudiwa pande hizi mbili zikigombana.

Nchi ya Sudan ilituma idadi kubw aya wanajeshi wake kwenye eneo la mpaka baada uvamizi wa vikosi vya Ethiopia, ambapo wanajeshi wanne waliuawa kwenye eneo la Al fashaqa.