ZIMBABWE-WFP

WFP yatiwa wasiwasi na hali ya chakula nchini Zimbabwe

WFP laonya kuhusu baada la njaa barani Afrika
WFP laonya kuhusu baada la njaa barani Afrika STEFAN HEUNIS/AFP/Getty Images

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) mshindi wa Tuzo ya amani ya Tuzo ya Nobel (WFP) limetoa wito kutoa fedha za dharura katika kipindi cha miezi sita ijayo, kuwasaidia raia milioni nne wa Zimbabwe wanaokabiliwa na njaa.

Matangazo ya kibiashara

Mgogoro wa kiuchumi ambao nchi imekuwa ikipatia kwa miaka 20 iliyopita umezidi kuwa mbaya pamoja na janga la COVID-19 na raia kwa sasa wanakabiliwa na ukosefu wa chakula wakati msimu wa wa kipwa unatarajia kuanza.

 

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linasema linahitaji kukusanya zaidi ya dola milioni 200, au karibu euro milioni 160, kwa msaada wa chakula wa haraka nchini Zimbabwe, hasa vijijini.

 

Miaka kadhaa mfululizo ya ukame tayari imedhoofisha usalama wa chakula nchini Zimbabwe na mavuno ya mwaka huu yameathiriwa tena. Kulingana na takwimu kutoka Wizara ya Fedha, uagizaji wa chakula katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka huu umeongezeka mara tatu ikilinganishwa na mwaka jana.

 

Wakati huo huo janga la Corona limedhoofisha uchumi ambao tayari unalegalega, na mfumuko wa bei ambao unasababisha bei za bidhaa mahitajio kupanda mara dufu. Mwaka 2020 kuliripotiwa watu milioni moja zaidi walioathiriwa na umasikini ikilinganishwa na mwaka 2019.

 

Hali kwa ujumla katika ukanda huo inatia wasiwasi, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa, tangu mwaka huu, zaidi ya watu milioni 40 walipatikana wakiwa na uhaba wa chakula kusini mwa Afrika.