SOMALIA-MAREKANI

Ipi hatma ya Somalia baada ya kuondoka vikosi vya Marekani

Vikosi vya kulinda amani nchini Somalia, AMISOM
Vikosi vya kulinda amani nchini Somalia, AMISOM Reuters/Feisal Omar

Vikosi vya Marekani nchini Somalia, vinatarajiwa kuanza kuondoka nchini Somalia kuanzia mapema mwaka 2021, baada ya agizo la rais anayemaliza muda wake Donald Trump.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, wanajeshi hao watakwenda katika kambi zisisofahamikika katika nchi za Afrika Mashariki.

Hivi karibuni rais wa Marekani, Donald Trump aliwaagiza karibu ya wanajeshi wote wa taifa hilo walioko nchini Somalia kurejea nchini mwao. Taifa hilo lina wanajeshi takriban mia saba wanaohudumu nchini Somalia ambao wamekuwa wakichangia juhudi za kulikabili kundi la kigaidi la Al Shabaab.

Marekani ilitengaza kupiga hatua kubwa katika kulikabili kundi hilo hali ambayo inaonekana kuchangia kuanza kuondoka kwa wanajeshi wake.

Mapema mwaka huu, Marekani ilikuwa tayari imewaondoa wanajeshi wake katika miji ya Bossaso na Galkayo nchini Somalia. Hata hivyo wengine walikuwa bado katika maeneo ya Kismayo, Baledogle, Shabelle na Mogadishu.

Trump vilevile anatarajiwa kuwaagiza wanajeshi walioko Afghanistan na Iraq kurejea Marekani huku Rais huyo akitarajiwa kuondoka uongozini rasmi mwezi Januari kumpisha Joe Biden.