MOROCCO-ISRAEL

Ndege ya kwanza ya kibiashara kati ya Israeli na Morocco yawasili Rabat

Ndege ya Kwanza ya Israel yatua Morocco.
Ndege ya Kwanza ya Israel yatua Morocco. JACK GUEZ / AFP

Ndege ya kwanza ya moja kwa moja ya kibiashara kati ya Israeli na Moroko imeanza shughuli zake leo Jumanne na mkwewe rais wa Merika Donald Trump, Jared Kushner, na mshauri wa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu wmesafiri na ndege hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ni ushahidi tosha kwamba uhusiano kati ya nchi hizi mbili unaelekea pazuri.

 

Baada ya Falme za Kiarabu, Bahrain na Sudan, Morocco imekuwa nchi ya nne katika ulimwengu wa Kiarabu kutangaza mwaka huu kurejesha uhusiano wake na Israel chini ya mwavuli wa Marekani.

 

"Nilikuwa hapa miezi michache iliyopita kwa safari ya ndege ya kwanza kwenda Falme za Kiarabu baada ya mafanikio haya ya kihistoria kuhusu amani. Tangu wakati huo, ndege za kibiashara zimekuwa zikisafiri mara kadhaa kwa siku kati ya nchi hizo mbili (...) , matumaini yangu ni kwamba ndege hii leo nchini Morocco inaimarisha hali kama hiyo, "almesema Bw. Kushner kwenye uwanja wa ndege wa Ben Gurion huko Tel Aviv.

 

"Katika kipindi cha miaka 75 iliyopita, Wayahudi na Waislamu walitengana, jambo ambalo sio la kawaida kwani pande hizi mbili ziliishi pamoja kwa karne nyingi katika ukanda huu (...) na tunachokiona leo ni ule uhusiano wa kale ambao umerudi tena, ” ameongeza mkwe wa rais wa Marekani na mtetezi wa mpango wa Trump kwa Mashariki ya Kati, uliokosolewa na Palestina.

 

Kabla ya janga la ugonjwa wa coronavirus, Morocco ilikuwa ikipokea kwenye ardhi yake watalii wa Kiyahudi kati ya 50,000 na 70,000 kila mwaka, wengi wao wakisafiri kwa ndege ya moja kwa moja kutoka Israeli.