ETHIOPIA

Abiy Ahmed aanzisha vita vipya nchini Ethiopia, kwenye mpaka wa Sudan

Waziri Mkuu wa Ethiopia  Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed © Tiksa Negeri / REUTERS

Wakati jeshi la Ethiopia limekuwa likipambana na chama kilioasi cha TPLF katika jimbo la Tigray kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu, tangu wiki iliyopita pia jeshi la Ethiopia limekuwa likikabiliana na jeshi la Sudan kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Abiy Ahmed ameamua kuanzisha operesheni mpya ya kijeshi katika jimbo la Benishandul Gumuz magharibi mwa nchi kwa lengo la kuyatimu makundi ya kigaidi lakini operesheni hii imezua hofu ya kutokea kwa vita kati ya Ethiopia na Sudan.

Benishandul Gumuz, jimbo lenye wakaazi zaidi ya milioni moja kutoka makabila tofauti, limeendelea kushuhudia visa vingi vya unyanyasaji na mauaji katika miezi ya hivi karibuni.

Jamii ya walio wachache ya Amhara wanaoishi katika mkoa huo ni miongoni mwa makabila yanayolengwa na mauaji hayo.

Serikali ya Addis Ababa inashtumu makundi mawili, TPLF na Oromo (OLF) kuchochea machafuko ambayo yamechochewa na makundi anayosema ni ya kigaidi.

Mapema wiki hii Abiy Ahmed alizuru jimbo la Benishandul Gumuz na kutangaza "mkakati maalum" wa kudhibiti jimbo hilo bila kutoa maelezo zaidi.

Waziri mkuu alikuwa ameandamana na mkuu wa jeshi, na kampeni za nyumba kwa nyumba tayari zimeanza.

Inahofiwa kwamba operesheni hii itakuwa na mwelekeo mkubwa wa kikabila kwa kuzingatia mizozo iliyopo kati ya jamii, pia kwa mtazamo wa maneno hasa yanayotumiwa na baadhi ya viongozi dhidi ya makabila ya Gumuz na Berta, walio wengi katika jimbo hilo.

Ikumbukwe kwamba jimbo hili ni la kimkakati kwa Addis Ababa kwa sababu huko ndiko kuna bwawa kubwa kwenye Mto Nile, ambalo ni bwawa kubwa zaidi barani Afrika.