JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

CAR: Hali ya utulivu yaripotiwa Bangui, milio ya risasi yasikika Boali

Vikosi vya usalama nchini jamhuri ya Afrika ya Kati wakilinda usalama.
Vikosi vya usalama nchini jamhuri ya Afrika ya Kati wakilinda usalama. RFI/Charlotte Cosset

Jamhuri ya Afrika ya Kati inakabiliwa na mvutano, siku nne kabla ya Uchaguzi wa Mkuu. Kwa karibu wiki moja sasa, muungano wa makundi yenye silaha umekuwa ukijaribu kuzuia uchaguzi huo zisifanyike na kusonga mbele kuelekea mji mkuu Bangui.

Matangazo ya kibiashara

Jumatano hii, Desemba 23 asubuhi, milio ya risasi imesikika karibu na mji wa Boali, kilomita mia moja kutoka mji mkuu, Bangui.

 

"Hali ni shwari huko Bangui", Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA amesema katika taarifa. Shughulii zimesitishwa kwenye barabara kuu, kwa sababu asubuhi ya leo, watu walikuwa na hofu baada ya uvumi kusambazwa kwamba mji mkuu utashambuliwa na waasi.

 

Uvumi huu umekanushwa tangu wakati huo. Hata hivo wakazi wa mji huo, hususan wanawake wakiwa na watoto mikononi, walionekana wakikimbilia kila sehemu kutafuta ulinzi, ikiwa ni pamoja na katikati ya jiji. Hii ni ishara kwamba wasiwasi umengezeka wakati uchaguzi wa Jumapili unakaribia. Wakati wa mchana, hali ya utulivu ilirejea.

 

Hivi karibuni Urusi na Rwanda, zilituma wanajeshi wake nchini humo kusaidia kuimarisha usalama.