MOROCCO

Morocco: Mfalme Mohammed VI apokea ujumbe wa kidiplomasia wa Israeli na Marekani

Mfalme wa 6 wa Morocco, akiwa na walinzi wake
Mfalme wa 6 wa Morocco, akiwa na walinzi wake REUTERS/Tiksa Negeri

Hatua ya Marekani ya kuchangia katika kurejesha uhusiano ya Morocco na Israel imeendelea kukaribishwa na watu kutoka tabaka mbalimbali ikiwa ni pamoja na taasisi mbalimbali nchini Morocco.

Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa Israeli na Marekani, uliyoongozwa na mkwewe rais wa Marekani Donald Trump, Jared Kushner ulifanya ziara nchini Morocco Jumanne hii, Desemba 22.

Ni kitendo ambacho kinarasimisha kuanza tena kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Israeli na Morocco.

Baada ya ndege ya kwanza kabisa ya kibiashara kufanya safari ya moja kwa moja kati ya Israeli na Morocco, ikiwa ni tukio la kihistoria ujumbe wa Marekani ukiongozwa na Jared Kushner na Meir Ben-Shabbat, mshauri wa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, ambaye aliwakilisha serikali ya Israeli walizuru makaburi ya wafalme Mohammed V na Hassan II, viongozi wawili mashuhuri sana nchini Israeli wamelala, na kisha walipokelewa na Mfalme Mohammed VI katika kasri la kifalme huko Rabat. Wakati uliosubiriwa kwa muda mrefu.

Mfalme Mohammed VI aliwapokea Jared Kushner, Meir Ben-Shabbat, mshauri wa Waziri Mkuu wa Israeli katika masuala ya usalama wa taifa na Avraham Joel Berkowitz, Msaidizi Maalum wa Donald Trump.

Mfalme Mohammed VI alimpongeza Jared Kushner kwa kazi iliyokamilishwa tangu ziara yake nchini Morocco, mwaka 2018, ambayo ilifanya iwezekane "kufanikisha mabadiliko haya ya kihistoria kwa kuzingatia uhuru wa Morocco na mafanikio haya ya amani katika Mashariki ya Kati" .

Azimio la pamoja la pande tatu lilisainiwa, ambapo Marekani inatambua uhuru wa Morocco katika eneo la Sahara na ambapo Morocco imejikubalisha kuanzisha tena uhusiano wake na Israeli.

Utawala wa kifalme nchini Morocco unatarajia kuidhinisha safari za moja kwa moja kati ya nchi hiyo na Israeli lakini pia kufungua ofisi za uhusiano kati ya Rabat na Tel Aviv, kwa wiki mbili zijazo. Mikataba kadhaa inayohusu ushirikiano wa kiuchumi, usalama, teknolojia na kilimo pia imetiliwa saini kati ya nchi hizi mbili.