TUNISIA

Tunisia yapinga kurejesha uhusiano na Israeli

Kais Saied rais wa Tunisia akiwa na Jean-Yves Le Drian Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa
Kais Saied rais wa Tunisia akiwa na Jean-Yves Le Drian Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa AFP

Tofauti na nchi nyingine za Kiarabu hivi karibuni, Tunisia imesema haina nia yoyote ya kurejesha uhusiano wake na Israeli, wizara ya mambo ya nje ya Tunisia imesema.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya Falme za Kiarabu, Bahrain na Sudan, Morocco ilijiunga na nchi za Kiarabu zilizoamua kurejesha uhusiano wao na serikali ya Israel chini ya mwavuli wa Marekani.

Taarifa ya Tunisia inajibu dhana kwamba nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika iko mbioni kufuata mfano huo, chini ya shinikizo kutoka kwa utawala wa Donald Trump.

Palestina imekuwa ikiyatuhumu makubaliano hayo na kuyataja kuwa usaliti kwa azma ya Palestina.

Mazungumzo kati ya Israel na Palestina yalikwama mara ya mwisho mnamo mwaka 2014 na rais wa Palestina Mahmoud Abbas alikataa uhusiano wowote wa kisiasa na serikali ya Trump akiituhumu kwa kuipendelea Israeli.