AFRIKA KUSINI

Virusi vipya: Nchi kadhaa zasitisha safari za ndege kutoka na kuelekea Afrika Kusini

Virusi vya Covid 19
Virusi vya Covid 19 NIAID-RML via AP

Mataifa zaidi yametangaza kusitisha safari za ndege kutoka na kuelekea nchini Afrika Kusini, baada ya taifa hilo kutangaza kuwa na maambukizi mapya ya virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya mataifa ambayo yametangaza kusitisha safari zake za ndege kutoka Afrika Kusini, ni Israeli, Ujurumani, Uswisi, Saudi Arabia na Uturuki, wakati huu taifa hilo likizidi kusajili idadi ya juu ya maambukizi na vifo.

Kwa mjibu wa maafisa wa afya kutoka Afrika Kusini, maambikizi hayo mapya kwa jina 501 V2, yanaambukizwa kwa kasi mno na ni tofauti na yale yanayorippotiwa nchini Uingereza.

Tayari wataalamu nchini humo wameanzisha uchunguzi kubaini iwapo chanjo zinazotolewa zina uwezo wa kukabili makali ya aina hii mpya ya maambikizi.

Serikali ya Afrika Kusini imetangaza masharti mapya ya kudhibiti maambukizi zaidi ikiwemo kufungwa kwa maeneo ambayo raia wanatangamana kwa wingi.

Hadi sasa Afrika Kusini imerekodi visa 930, 711 vya maambukizi na vifo 24, 907, vilivyotokana na Corona.