SUDAN-ETHIOPIA

Mgogoro mpakani: Ujumbe wa Ethiopia nchini Sudan

Ramani inaonesha nchi ya Sudan na Ethiopia
Ramani inaonesha nchi ya Sudan na Ethiopia Reuters

Ujumbe wa Ethiopia unazuru Sudan katika jaribio la kumaliza mzozo unaoendelea kutokota kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili.

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo yaliyofanyika Jumatatu huko Khartoum yanalenga kuweka upya mpaka katika miezi ijayo.

Baada ya kuwasili Khartoum, Waziri wa Mambo ya nje wa Ethiopia, Demeke Mekonnen aliita mtazamo wa Sudan kuwa "hauna urafiki".

Tangu Novemba 9, tumeshuhudia visa vya uporaji wa bidhaa vya kilimo kutoka Ethiopia, kambi zao ziliharibiwa na mavuno yao yameharibiwa," amesema.

Maafisa wa serikali ya Sudan wamebaini kwamba mnamo Desemba 15, wanajeshi wao waliokuwa wakipiga doria walishambuliwa na wanamgambo wa Ethiopia, na kuua 4 na kujeruhi wengine kadhaa.

Lakini pamoja na taarifa hizi ambapo kila upande umekanusha, wajumbe wa Sudan na Ethiopia wamesema wanataka kuafikianaili waweze kusuluhisha kwa amani mzozo huu wa mpakani.

Pia kwenye ajenda, vita dhidi ya shughuli haramu katika mkoa huo na usalama wa wenyeji ambao wanaishi katika eneo hilo.

Mawaziri wakuu wa Ethiopia na Sudan, ambao walikuwa tayari wamekutana Jumapili kando mwa mkutano wa IGAD huko Djibouti, walisema wanataka kurejesha utulivu katika eneo la mpaka wa el-Fashaga ambapo jeshi la Sudan limekuwa likiendesha mashambulizi kwa wiki kadhaa dhidi ya wanamgambo wa Ethiopia.

Pande hizo mbili zimekaribisha uhusiano wao "wa kirafiki na wa kindugu".

Walikubaliana juu ya mkutano ujao huko Addis Ababa na kutangaza kwamba ujumbe utatumwa baadaye ili kuweka upya mpaka kati ya nchi hizo mbili.