TUNISIA

Miili Ishirini ya wahamiaji katika pwani ya Tunisia

Wahamiaji wakiwa Baharini, wanasafiri katika mazingira hatarishi
Wahamiaji wakiwa Baharini, wanasafiri katika mazingira hatarishi AFP

Miili 20 ya wahamiaji kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara zimeokolewa katika pwani ya Sfax, pwani ya mashariki mwa Tunisia, baada ya boti lao kuzama, Mohamed Zekri, msemaji wa wizara ya ulinzi ameliambia shirika la habari la AFP.

Matangazo ya kibiashara

Wahamiaji wengine watano ambao walikuwa kwenye boti hilo waliokolewa na shughuli za kutafuta miili mingine bado zinaendelea, Zekri ameongeza bila kutoa maelezo zaidi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani Khaled Hayouni amesema kwa upande wake kwamba miili 15 ya wahamiaji imepatikana "kwa sasa" na kwamba watu watano wameokolewa wakiwa hai.

Kulingana na Khaled Hayouni, boti hilo liliondoka katika eneo la Sidi Mansour, katika mkoa wa Sfax, kwa kujaribu kuingia katika pwani ya Italia kinyume cha sheria.