CONGO

Rais Sassou Nguesso ataka uchaguzi kufanyika 'kwa uwazi na amani'

Rais wa Jamhuri ya Congo Brazaville Denis Sassou-Nguesso.
Rais wa Jamhuri ya Congo Brazaville Denis Sassou-Nguesso. EVGENIA NOVOZHENINA / POOL / AFP

Rais wa Congo Denis Sassou Nguesso amesema anataka uchaguzi ufanyike "kwa uwazi na amani" ifikapo Machi 21 nchini mwake, ambaye pia anataka kabla ya yote "kwanza chanjo dhidi ya COVID-19 ianze kutolewa.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi ujao wa urais umepangwa kufanyika "Machi 21, 2021," Sassou Nguesso amesema wiki hii katika hotuba kwa taifa mbele ya wabunge.

"Tunapaswa kufanya uchaguzi ujao kwa uwazi na amani, kwa kuheshimu muda uliowekwa na katiba ya sasa," amesema rais Sassou Nguesso

Bw. Sassou Nguesso, mwenye umri wa miaka 77, ambaye yuko madarakani kwa miaka 36, anapewa nafasi kubwa ya kushinda katika uchaguzi huo.