ETHIOPIA

Ethiopia: Uchaguzi wa wabunge kufanyika Juni 2021

Waziri Mkuu wa Ethiopia  Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed © Tiksa Negeri / REUTERS

Ethiopia itafanya uchaguzi wa wabunge mnamo Juni 5, 2021, Tume ya kitaifa ya Uchaguzi imesema Ijumaa leo Ijumaa wakati nchi hiyo inaendelea kukabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo ambao hapo awali ulipangwa kufanyika mnamo mwezi Agosti, uliahirishwa kwa sababu ya janga la COVID-19.

Ethiopia ambayo ni nchi ya pili yenye watu wengi barani Afrika imeendelea kukumbwa na uhasama wa mara kwa mara tangu Abiy Ahmed, mwanzilishi wa Chama cha Mafanikio, alipoingia madarakani mnamo mwaka 2018 na kuongeza kasi ya mageuzi ya kidemokrasia ambayo yalilegeza udhibiti wa kitaifa kuhusu uhasama baina ya majimbo.

Kaskazini mwa nchi hiyo, jeshi la Ethiopia liliongoza mashambulizi mwezi uliopita dhidi ya waasi katika eneo lililojitenga la Tigray, na kudai kuwa limewatimuwa waasi katika jimbo hilo. Mapigano hayo yamesababisha zaidi ya wakaazi 950,000 kutoroka makaazi yao.

Uhamasishaji wa wanajeshi wa Ethiopia katika eneo hilo lenye mzozo umeongeza hofu ya kukosekana kwa usalama katika maeneo mengine yasiyokuwa na utulivu.

Wiki hii wanajeshi wa Ethiopia walipambana na watu wenye silaha waliohusika katika shambulio baya katika mkoa wa magharibi wa Benishangul-Gumuz, na kuwaua 42 kati yao na kuteka silaha