NIGER

Hali ya wasiwasi yatanda siku moja kabla ya uchaguzi Niger

Mahamadou Issoufou, rais anayemaliwa muda wake nchini  Niger.
Mahamadou Issoufou, rais anayemaliwa muda wake nchini Niger. ©RFI

Hali ya usalama nchini Niger inaendelea kuwa hatarini nchini kufuatia vitisho vya makundi ya kijihadi, wakati nchi hiyo inafanya Uchaguzi Mkuu Jumapili Desemba 27.

Matangazo ya kibiashara

Makundi ya wanamgambo aw Kiislamu yanaripotiwa katika jimbo la  Ziwa Chad na kwenye eneo la mpakani na Mali.

Viongozi wa kisiasa wanaofanya kampeni wamelichukulia suala la usalama kuwa moja ya masuala muhimu yanayotakiwa kushughulikiwa haraka iwezekanavyo iwapo watakuwa madarakani.

Licha ya zoezi la kampeni kwenda vizuri nchini kote Niger, wanajihadi wanasema bado wako na watahakikisha uchaguzi huo haufanyiki.

Wanajihadi hao walifanya mashambulio mawili katika siku za hivi karibuni. Katika shambulio la kwanza, huko Toumour katika jimbo la Ziwa Chad, Boko Haram iliua raia 34, wakimbizi kutoka Nigeria, Desemba 13.

Katika shambulio la pili, mapema wiki hii karibu na mpaka wa Mali, wanajeshi waliokuwa wakipiga doria walivamiwa na kundi la wanajihadi. Katika tukio hilo wanajeshi watano wa Mali na wanajihadi wanne waliuawa.