DRC

DRC: Félix Tshisekedi akutana kwa mazungumzo na Moïse Katumbi na Jean-Pierre Bemba

Rais wa DRC, Félix Tshisékédi.
Rais wa DRC, Félix Tshisékédi. ISSOUF SANOGO / AFP

Rais wa DRC Félix Tshisekedi anaendelea kukutana na wanasiasa mbalimbali wa upinzani katika kujaribu kuunda muungano wa kisiasa, baada ya kuvunja muungano uliokuwepo wa FCC-CASH.

Matangazo ya kibiashara

Jumamosi, Desemba 26 jijiniKinshasa, rais Tshisekedi aliwapokea kwa mazungumzo Moïse Katumbi na Jean-Pierre Bemba ambao ni kutoka muungano wa upinzani wa Lamuka. Hadi wakati huu, wanasiasa hawa wa kubwa katika siasa ya DR Congo bado ni viongozi wa kambi ya upinzani.

Mara tu baada ya kutangazwa kuvunjika kwa muungano wa kisiasa kati ya Félix Tshisekedi na Joseph Kabila, mwanzoni mwa mwezi Desemba, Moïse Katumbi na Jean-Pierre Bemba waliamua kumuunga rais wa sasa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Moïse Katumbi na Jean-Pierre Bemba waliwasili jijini Kinshasa Jumamosi. Vigogo hao wawili wa muungano wa wa upinzani Lamuka hawakutoa taarifa kwa vyombo vya habari. Mkutano na Felix Tshisekedi ulidumu saa tatu, bila mjumbe kutoka serikali kuhudhuria. Kulikuwa na wanasiasa watatu tu katika moja ya afisi za kibinafsi za rais jijini Kinshasa.

 

Kulingana na mshauri wa rais, mazungumzo yalikwenda vizuri na walijadili kuhusu mabadiliko ya hali ya kisiasa nchini DRC, na kusisitiza hasa juu uwezekano wa kuunda muungano mpya wa kisiasa.

Wakati huo huo, rais wa sasa anaendelea kupanua ushawishi wake. Kabla ya mazungumzo na vigogo wawili wa Lamuka, Jean-Pierre Bemba na Moïse Katumbi, alipokea wajumbe kutoka makundi manne ya wabunge, waliokuwa upande siku chache zilizopita wa muungano wa FCC wa Joseph Kabila.