NIGER

Raia wa Niger, wapiga kura katika uchaguzi wa kihistoria

wafanyakazi wa tume ya uchaguzi Niger, wakihakiki masanduku ya kura
wafanyakazi wa tume ya uchaguzi Niger, wakihakiki masanduku ya kura Gulf Times

Wananchi wa Niger wanapiga kura leo Jumapili Desemba 27 kumchagua rais na wabunge katika uchaguzi mkuu.Wapiga kura milioni 7 wanashiriki uchaguzi huo kumchagua rais mpya na wabunge 171 watakaohudumu katika awamu mpya ya uongozi.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mara ya kwanza uchaguzi huu utahusisha wagombea wengi zaidi wa kuwania kwenye kiti cha urais. Jumla ya wagombea 30 wanashiriki kinyang'anyiro hiki cha urais.

 

Wananchi wa Niger wana matumaini ya kuweka historia leo Jumapili watakapo kwenda kupiga kura katika uchaguzi wa rais na bunge ambao kwa mara ya kwanza utaruhusu kukabidhiana madaraka kwa amani tangu kupata uhuru miaka 60 iliyopita kutoka Ufaransa.

 

Rais wa zamani Mahamane Ousmane, Salou Djibo, ambaye aliwahi kuwa rais wa kipindi cha mpito baada ya mapinduzi, mawaziri wakuu wa zamani Amadou Boubacar Cisse na Seini Oumarou, Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani Bazoum Mohamed, na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje Ibrahim Yacoubou ni miongoni mwa wagombea katika uchaguzi huo wa urais.

Hata hivyo wagombea kiti cha urais wako 17 ambao wanashindana kuchukua nafasi ya Mahamadou Issoufou anaekamilisha muhula wake wa pili

Rais wa sasa, Mahamadou Issoufou, hatowania kwenye nafasi hiyo kwa sababu tayari  amekamilisha muhula wake wa 2 madarakani.

Kiongozi wa upinzani Hama Amadou, sio miongoni mwa wagombea kwenye kiti hiki kwa sababu ya hukumu aliyopewa na amekuwa akimpigia debe Ousmane kwa kuhimiza raia wampigie kura.

Hama Amadou wa chama cha upinzani cha Lumana aliyekuwa Spika wa zamani na Waziri Mkuu mara mbli anayechukuliwa kuwa mshindani mkubwa kwenye uchaguzi wa urais ameondolewa kwa madai kwamba alihukumiwa kifungo cha miezi 12 kutokana na kashfa ya biashara haramu ya Watoto hapo mwaka 2017.

Kutakuwa na duru ya pili pindi hakuna mgombea aliyepata zaidi ya asilimia 50 za kura.

Niger ni mojawapo ya mataifa maskini duniani licha ya utajiri mkubwa wa madini, inakabilwa na matatizo makubwa ya kiuchumi na hasa mashambulio ya wanamgambo wenye itikadi kali za kislamu kutoka nchi jirani za Mali na Nigeria.