DRC-SIASA

DRC: Magavana wa mikoa 26 kukutana kwa mazungumzo na rais Tshisekedi

Rais wa DRC  Félix Tshisekedi
Rais wa DRC Félix Tshisekedi Sumy Sadurni / AFP

Nchini DRC, magavana wa mkoa ishirini na sita wameitwa Kinshasa kwa mkutano mbele ya rais Félix-Antoine Tshisekedi. Mada ya mkutano huu: "utawala wa mikoa katika mazingira ya sasa ya kidemokrasia, changamoto na fursa".

Matangazo ya kibiashara

Mkutano wa magavana unakuja katika kilele cha mzozo ndani ya muungano wa kisiasa wa FCC-CACH , ambapo wengi kutoka muungano wa FCC wa Joseph Kabila wameanza kujiunga na muungano wa rais Tshisekedi wa CASH.

Mkutano huu ni wa pili wa aina yake katika kipindi cha miaka mitano cha kwanza cha mrithi wa Kabila na unakuja baada ya mfululizo wa matukio ambayo yameidhoofisha kambi ya FCC ya Joseph Kabila.

Kwanza, kulikuwa na mgawanyika katika muungano huo kabla ya kwa Jeanine Mabunda, spika wa Bunge na ofisi yake yote, iliyokuwa ikiundwa hasa na maafisa kutoka FCC kuvunjwa.

Kikwazo cha pili kwa FCC: barua kutoka kwa maseneta sita wanaomuunga mkono Kabila ambao wamemfahamisha kiongozi huyo wa zamani kuhusu shida kadhaa zinazokabili muungano huo wa FCC na ambao wanaomba kuondolewa kwa viongozi wake.

Katika jaribio la kuokoa kile kinachoweza kuokolewa, tume ya kutatu mgogoro iliundwa na rais wa zamani Joseph Kabila... Tume hii, itaendelea na mashauriano yake na wabunge kutoka muungano huo katika ngazi ya kitaifa na wakuu wa makundi ya kisiasa kujaribu kuelewa hali inayojiri katika muungano wa FCC na kujaribu kuunganisha tena kambi ya Kabila, amesema Raymond Tshibanda, mwenyekiti wa tume hiyo.