AFRIKA KUSINI

Afrika Kusini yatangaza makataa mapya ya kukabiliana na maambukizi ya Covid 19

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa. Phill Magakoe / AFP

Nchi ya Afrika Kusini, imetangaza makataa mapya zaidi kwa mara nyingine ili kukabiliana na ongezeko la maambukizi ya Covid 19 ambayo yamechangiwa na mlipuko wa virusi vipya vya Covid 19. 

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa makataa mapya yaliyotangazwa ni pamoja na kuzuiwa kwa mikusanyiko ya ndani na nje pamoja na makataa ya kutembea usiku itakayoanza satatu usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi.

Ni wafanyakazi wenye vibali, wakiwemo wahudumu wa afya, maofisa usalama na wengine wa misaada, ndio watakaoruhusiwa kutembea.

Katika hotuba yake rais nCyril Ramaphosa amesema "Kuanzia sasa ni lazima kwa kila mtu kuvaa barakoa katika maeneo ya uma, mtu ambaye hatavaa barakoa atakuwa akitenda kosa," alisema.

"Katika kuhukumiwa watakabiliwa na kifungo cha miezi 6 jela au kulipa faini au vyote kwa pamoja."

Rais Ramaphosa, pia amesema huduma zisizo za muhimu kama maduka, migahawa, vilabu vya pombe na vituo vya utamaduni, sasa vitafungwa saa mbili usiku, huku maduka ya vileo hayataruhusiwa.

kwa mujibu wa rais Ramaphosa, makataa haya mapya yatadumu kwa siku 14 na yatafanyiwa tathmini kabla ya kuamua yaondolewe au la.