MALI

Wanajeshi watatu wa Ufaransa wauawa katika operesheni katikati ya Mali

Mwanajeshi wa Ufaransa nchini Mali
Mwanajeshi wa Ufaransa nchini Mali Reuters

Wanajeshi watatu wa Ufaransa wa kikosi cha Barkhane wameuawa katika operesheni nchini Mali siku ya Jumatatu, wakati gari lao lililoposhambuliwa kwa kifaa cha kulipuka katika mkoa wa Hombori, ikulu ya Elysée imesema.

Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi watatu wa Ufaransa wa kikosi cha 1 cha Thierville-sur-Meuse walipoteza maisha Jumatatu, Desemba 28.

Gari lao la kivita lilishambuliwa kwa "kifaa cha kulipuka" Jumatatu asubuhi wakati walikuwa wakisindikiza msafara wa magari kati ya Hombori na Gossi, katika Jangwa la Gourma katikati-mashariki mwa nchi ya Mali karibu na mpaka wa Burkina Faso.

Hombori ni eneo la kimkakati, kwani kunapita barabara kuu , inayounganisha mji wa Kona katikati mwa nchi na Gao Mashariki , ambapo kunapatikana kundi la kigaidi lenye silaha linalojulikana kwa jina la RVIM (Mkusanyiko wa ushindi wa Uislamu na Waislamu).

Kulingana na mkuu wa majeshi ya Ufaransa, vikosi vya Barkhane vilipelekwa mara moja baada ya tukio hilo kutokea.

Kulingana na Wizara ya majeshi, wanajeshi waliingilia kati katika eneo ambalo makundi ya kigaidi yanaendesha mashambulizi dhidi ya raia na kutishia utulivu wa ukanda huo. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Ofisi ya rais wa Jamhuri inasisitiza azma ya Ufaransa ya kuendelea na mapambano dhidi ya ugaidi.

Majeshi ya Ufaransa na Mali yalikuwa yameanzisha hivi karibuni katika eneo hilo operesheni ya pamoja ya ushirikiano ya mwezi mmoja, ili kuongeza ushirikiano wao, kwa kuchukua hatua na kulinda raia kwa pamoja.