DRC-USALAMA

Watu 34 waliuawa Mashariki mwa DRC kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita

Wanajeshi wa DRC wakiwa Mashariki mwa nchi hiyo
Wanajeshi wa DRC wakiwa Mashariki mwa nchi hiyo Reuters

Raia 34 waliuawa katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha katika jimbo la Kivu Kaskazini  na Kusini, Mashariki mwa DRC kwa mujibu wa ripoti ya watalaam wa masuala ya usalama kutoka Security Barometer of Kivu (KST).

Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo inaeleza kuwa kati ya Novemba 29 hadi Desemba 12, watu hao waliuawa huku wengine 19 wakitekwa na watatu wakijeruhiwa katika majimbo ya mawili.

Kati ya visa vitatu vilivyoripotiwa na watalaam hao, vitatu vilitokea katika Wilaya ya Beni katika jimbo la Kivu Kaskazini huku watu 25 wakiuawa baada ya kushambuliwa na kundi la waasi la ADF.

Huko Rutshuru, watu wasiofahamika, waliwateka nyara wanaume wawili na wasichana watatu, na kutaka kikombozi cha Dola Elfu tano ili kuaaachia huru.

Kundi la ADF linaendelea kuwa hatari sana katika majimbo hayo mawili na linashtuliwa kutekeleza mauaji ya zaiida ya watu mia nane, kila mwaka.

Rais wa nchi hiyo Felix Thisekedi amekuwa akiahidi jeshi la nchi hiyo na lile la Monusco kushinda kundi hilo na makundi mengine lakini hilo halijafanyika.