COTE D'IVOIRE-SIASA

Cote d'Ivoire: Uchaguzi wa wabunge kufanyika Machi 2021

Rais wa Cote Dvoire Alassane Ouattara
Rais wa Cote Dvoire Alassane Ouattara RFI/France24

Uchaguzi wa wabunge wa nchini Côte d'Ivoire utafanyika mnamo Machi 6. Agizo hilo limepitishwa na Baraza la Mawaziri. Kufikia tarehe hiyo wapiga kura watawachagua wabunge wapya 255.

Matangazo ya kibiashara

Serikali inaelezea chaguo la tarehe hiyo kwa kuheshimu kalenda ya uchaguzi kama inavyosema katiba, hasa tarehe ya ufunguzi wa kikao kijacho cha bunge, kilichopangwa kufanyika mwezi Aprili.

Tangazo hili linakuja siku moja baada ya kumalizika kwa mazungumzo ya kisiasa kati ya chama tawala na vyama vya upinzani.

Desemba 26 Tume huru ya Uchaguzi (CEI) ilipendekeza uchaguzi ufanyike Machi 6, 2021 ikiibaini kwamba wagombea watachukuwa fomu za kuwania katika uchaguzi huo wiki ijayo hadi Januari 20.

CEI ilipendekeza tarehe hiyo siku chache baada ya kuanza kwa mazungumzo ya kisiasa kati ya serikali, vyama vya upinzani na asasi za kiraia.