ETHIOPIA

Ripoti: Maafisa wa usalama nchini Ethiopia waliwauwa watu 75

Wanajeshi wa Ethiopia
Wanajeshi wa Ethiopia REUTERS/Tiksa Negeri

Tume ya Haki za Binadamu nchini Ethiopia katika, ripoti yake iliyotolewa siku ya Ijumaa inaeleza kuwa maafisa wa usalama, waliwauwa watu zaidi ya 75 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 200 wakati wa makabiliano ya kikabila mwezi Juni na Julai mwaka 2020, baada ya kuuawa kwa mwanamuziki maarufu Hachalu Hundessa.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo inaeleza kuwa, katika makabiliano hayo, jumla ya watu  123 waliuawa na wengine zaidi ya 500 walijeruhiwa katika mapigano hayo mabaya ya kikabila mwaka 2020.

Aidha, imebainika kuwa baadhi ya watu waliouawa walikatwa vichwa, huku wengine wakiteswa hadi kupoteza maisha na miili yao ikatupwa barabarani.

Mauaji hayo yalichochewa kufuatia kuuwa kwa mwanamuziki maarufu singer Hachalu Hundessa, ambaye hadi kuuawa kwake kwa kupigwa risasi alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali huku akishinikiza mageuzi nchini humo.

Kabila lililolengwa ni lile la Amhara katika mzozo ambao ulisababisha watu zaidi ya Elfu sita kuyakimbia makwao.

Makabiliano ya kikabila, linasalia suala tata nchini Ethiopia, taifa ambalo linaongozwa na Waziri Mkuu Abiy Ahmed, ambaye mwezi Novemba mwaka uliopita, aliagiza operesheni dhidi ya vikosi vya jimbo la Tigray.