NIGER-UCHAGUZI

Mzunguko wa pili wa Uchaguzi wa urais nchini Niger, kufanyika mwezi Februari

Bazoum Mohammed na  Mahamane Ousmane kuchuana katika mzunguko wa pili wa urais nchini Niger
Bazoum Mohammed na Mahamane Ousmane kuchuana katika mzunguko wa pili wa urais nchini Niger RFI Hausa

Mgombea wa urais wa chama tawala nchini Niger, Mohamed Bazoum atachuana na rais wa zamani Mahamane Ousmane katika mzunguko wa pili wa uchaguzi mwezi Februari.

Matangazo ya kibiashara

Hili limebainika baada ya Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka uliopita, siku ya Jumamosi na mshindi wa mzunguko wa kwanza kutopatikana.

Bazoum ameongoza mzunguko wa kwanza kwa kupata ushindi wa asilimia 39.33 na kushindwa kufika asilimia 50, huku rais wa zamani Ousmane akipata asilimia 17.

Tume ya Uchaguzi imesema mzunguko wa pili wa kumtafuta rais wa nchi hiyo, utafanyika tarehe 21 mwezi Februari, baada ya Mahakama ya Katiba kuidhinisha matokeo ya uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka uliopita.

Mshindi atachukua nafasi ya rais Mahamadou Issoufou , anayeondoka madarakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili na hatua hii inatarajiwa kuwa makabidhiano ya amani kwa viongozi wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa mara ya kwanza tangu ilipopata uhuru mwaka 1960.