JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Uchaguzi: Hali ya usalama yatisha kabla ya kutangazwa matokeo ya awali

Mpiga kura nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati
Mpiga kura nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Centre for Humanitarian Dialogue

Wakati matokeo ya awali ya uchaguzi yanatarajiwa kutangazwa Jumatatu, Januari 4 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, muungano wa makundi ya waasi unaendelea na mapigano kwa karibu wiki ya tatu nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Muungano wa waasi ulidaiwa kuanzisha mapigano kwa lengo la kuzuia kufanyika kwa uchaguzi. Siku ya Jumapili, hali ilikuwa bado tete nchini humo.

Siku ya Jumapili asubuhi, muungano wa waasi ulivamia mji wa Bangassou, Kusini-Mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Jioni, taarifa kuhusu hali usalama katika mji huo zilitofautiana.

Mkuu wa tume ya Umoja aw Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA, Mankeur Ndiaye, alihakikisha kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba kikosi cha MINUSCA kinadhibiti mji wa Bangassou na kinafanya doria kali.

Wakati huo huo, mkuu wa mji wa Bangassou alihakikisha kuwa vikosi vya Afrika ya Kati, wanajeshi kutoka Urusi na vile vile viongozi kadhaa walikimbilia katika katika kambi ya masheji ya Minusca. Alibaini kwamba mji huo unadhibitiwa na makundi ya waasi.

Hata hivyo MINUSCa imebaini kwamba wapiganaji watano wameuawa na wanajeshi wawili wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamejeruhiwa katika mji wa Bangassou.

Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa pia omeongeza kuwa watu nane kutoka upande wa waasi, CPC (Muungano wa Wazalendo wa Mabadiliko) wameuawa katika mapigano ambayo yalitokea katika mji wa Damara, mji ulio Kusini Magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jumamosi.

Watu wengi wenye silaha wameonekana katika mji wa Bossembele, kulingana na vyanzo kutoka eneo hilo. Kwa upande mwingine, vyanzo vya usalama vinahakikisha kuwa wapiganaji kadhaa wameonekana kilomita zaidi ya kumi na mji wa Bangui.

Kama mji mkuu na sehemu kubwa ya nyingi kulikuwa na utulivu siku ya Jumapili, miji mbalimbali ilikuwa na wasiwasi. Wakazi katika maeneo kadhaa wameelezea hofu yao kuhusiana na kudodora kwa usalama baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi.

Katika muktadha huu, Waziri Mkuu Firmin Ngrebada Jumapili alitoa wito kwa waandishi wa habari kutanguliza masilahi ya kitaifa na akaonya vituo vya redio vya kibinafsi ambavyo "vitaendelea kueneza habari za uwongo na kutetea uasi."