JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

CAR: Kiwango cha ushiriki chaweka mashakani uchaguzi baada ya nusu ya wapiga kura kuzuia

Faustin Archange Touadéra rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
Faustin Archange Touadéra rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati REUTERS/Sergei Karpukhin

Kiwango rasmi cha ushiriki kilichotangazwa Jumatatu jioni kilikuwa 76.31% kulingana na hesabu za Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (ANE), licha ya kutozingatia nusu ya wapiga kura, sawa na wapigakura 910,000 kati ya jumla ya wapiga kura milioni 1.8 waliojiandikisha ambao walizuiwa kupiga kura.

Matangazo ya kibiashara

Katika maeneo mbalimbali watu hawakupiga kura kwa sababu mbalimbali. katika baadhi ya maeneo zoezi la kupiga kura halikufanyika, na katika maeneo mengine kadi za kupigia kura zilichomwa," amebaini Théophile Momokoama, mmoja wa maafisa wa Tume ya Uchaguzi ANE amesema.

"Sio kosa letu lakini ni kosa la wale ambao hawakutaka uchaguzi ufanyike" amesema kiongozi wa kampeni ya rais anayemaliza muda wake, akibaini hata hivyo kwamba: "Uchaguzi ulifanyika, kwa hiyo raia waliamua iwe hivyo.

Tungependa tupate kura nyingi zaidi. Nina uhakika kwamba hali ya usalama ingelikuwa nzuri nchini kote na kuachia raia wajieleze kwa uhuru, ushindi ungeliukuwa wa juu zaidi kuliko huu ambao tumepata. "

Wakati huo huo upinzani tayari umetangaza kwamba utakata rufaa kwa Mahakama ya Katiba hasa juu ya suala hili. Jumatatu asubuhi, katika barua iliyoandikiwa Tume ya Uchaguzi, wagombea 9 wa upinzani walishutumu ukosefu wa "haki" katika uchaguzi huo, lakini pia "uwazi" wakati wa zoezi la kuhesabu kura na kukusanya matokeo, "kura nyingi zilijazwa" katika masanduku ya kura ”, ugumu kwa wawakilishi wao kupata nakala ya karatasi za matokeo jioni ya siku ya uchaguzi.

Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ilimtangaza rais anayemaliza muda wake Faustin-Archange Touadéra kuwa mshindi katika duru ya kwanza baada ya kujikusanyia asili mia  53.92% ya kura, kulingana na matokeo ya jumla.

Kwa mujibu wa matokeo hayo kiongozi wa upiunzani Anicet-Georges Dologuélé alipata asilimia 21.01, akifuatiwa na mwanasiasa mwengine Martin Ziguele katika nafasi ya tatu ambaye amepata asilimia 7.46%.

Upinzani una siku 3 tangu kutangazwa kwa matokeo ya awali ya uchaguzi kukata rufaa kwa Mahakama ya Katiba, ambayo kwa upande wake ina hadi Januari 19 kuzichunguza na kutangaza matokeo ya mwisho.