ETHIOPIA

Ethiopia: Madai ya uwepo wa vikosi vya Eritrea katika jimbo la Tigray yathibitishwa

Jeshi la Ethiopia
Jeshi la Ethiopia REUTERS/Tiksa Negeri/File Photo

Ethiopia sasa imekuwa katika mgogoro na jimbo la Tigray kaskazini mwa nchi hiyo kwa miezi miwili sasa, vyanzo kadhaa vinaripoti mapigano mengi katika maeneo ya vijijini.

Matangazo ya kibiashara

Miezi miwili ya mapigano, lakini pia miezi miwili ya kukatwa kwa intaneti, hali ambayo inasababisha ugumu katika kuchunguza hali halisi ya mambo katika jimbo hilo.

Hivi karibuni Marekani ilisahihisha madai ya uwepo wa wanajeshi wa Eritrea Tigray, madai ambayo yamethibitishwa pia na serikali ya mpito katika jimbo la Tigray iliyowekwa na serikali kuu ya Addis Ababa.

Meya wa mji mkuu wa mkoa Mekele amekuwa wa kwanza kuvunja mwiko. Ataklti Haileselassie amesema ndio, wanajeshi wa Eritrea walipigana vizuri huko Tigray, kwa mwaliko wa Addis Ababa.

Kulingana na meya wa mji mkuu wa mkoa Mekele, msaada huu wa Eritrea ulikuwa wa lazima kwa sababu chama cha Tigray cha TPLF kilikuwa kimeangamiza makao makuu ya jeshi huko Kaskazini ikimaanisha sehemu kubwa ya jeshi la Ethiopia.

Taarifa hii ni mshangao mkubwa wakati Waziri Mkuu Abiy Ahmed na utawala wake wamekuwa wakikanusha madai ya uwepo wa wanajeshi wa Eritrea katika jimbo la Tigray. Huko Asmara, serikali ya Isaias Afwerki, ingawa ni adui wa karibu wa TPLF, pia imeendele kukana kuingilia kati kijeshi katika jimbo la Tigray.

Lakini tuhuma za kwanza zilikuja wakati Abiy Ahmed alipoishukuru Eritrea kwa msaada wake wa vifaa vya jeshi mwishoni mwa mwezi Novemba.

Wakati huo huo, wakimbizi wanaopita Sudan walishuhudia uwepo wa wanajeshi wa Eritrea katika jimbo la Tigray. Madai haya baadaye yalithibitishwa na Marekani na wanadiplomasia wengine.