MALI

Kundi la GSM lakiri kuhusika na mauaji ya wanajeshi wawili wa Ufaransa Mali

Mwanajeshi wa Ufaransa nchini Mali
Mwanajeshi wa Ufaransa nchini Mali Reuters

Kundi la Qaeda linaloendeleza mashambulizi yake Kaskazini mwa bara la Afrika, limedai kuwauwa wanajeshi wawili wa Ufaransa ambao gari lao lilikanyaga bomu lililotegwa ardhini, Mashariki mwa Mali.

Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo linalojiita GSM, linadai lilitekeleza shambulizi hilo wakati gari la wanajeshi hao waliipokuwa wanapita, kwa mujibu wa jarida lake la Propaganda linalofahamika kama Al-Zallaqa.

Wanajeshi hao wa Ufaransa walikuwa katika operesheni ya kiusalama katika jimbo la Menaka waliposhambuliwa, na tukio hili lilijiri baada ya hsambulizi lingine kama hili na kuwauwa wanajeshi wengine watatu wa Ufaransa.

Tangu mwaka 2013, wakati Ufaransa ilipopeleka wanajesji Wake nchini Mali kusaidia katika vita dhidi ya makundi ya kijihadi, wanajeshi Wake 50 sasa wamepoteza maisha.

Ufaransa ina wanajeshi wake 5,100 ambao wanashiriki katika opereheni inayofahamika kama Barkhane kupambana na makundi ya kijihadi katika êneo la Sahel, linaloundwa na mataifa kama Mauritania, Chad, Mali, Burkina Faso na Niger.