DRC-USALAMA

Rais Tshisekedi azindua chuo cha kwanza cha mafunzo ya kivita DRC

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisékédi.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisékédi. Tchandrou Nitanga / AFP

Rais wa DR Congo Félix Tshisekedi amefungua chuo cha kwanza cha mafunzo ya kivita, ikiwa ni chuo cha pili cha aina hiyo katika ukanda wa Afrika ya Kati, kulingana na ikulu ya rais nchini DRC.

Matangazo ya kibiashara

Chuo hiki cha kiwango cha tatu ni matokeo bora ya ushirikiano kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Ufaransa.

Mradi huu ni matunda ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Ulaya na Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian, mwezi Mei 2019.

Wakati huo nchi hizo mbili zilikuwa ziliafikiana kufanya kazi pamoja katika kuunda chuo  cha mafunzo ya kivita kwa lengo la kuwapa elimu ya hali ya juu maafisa wa jeshi nchini humo ili kuboresha hali ya usalama.

Chuo hiki kilizinduliwa Jumanne wiki hii na rais Felix-Antoine Tshisekedi akiandamana na Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga.

Hayo yanajiri wakati hali ya usalama inaendelea kuzorota kila kukicha katika mikoa ya Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, ambapo makundi ya wapiganaji yamekuwa yakiua watu wasio kiuwa na hatia.