SENEGAL

Senegal yatangaza hali ya hatari kupambana na virusi vya Corona

Janga la Corona
Janga la Corona NEXU Science Communication | Reuters

Rais wa Senegal Macky Sall ametangaza hali ya hatari ili kukabiliana na kuongezeka kwa maambukizi mapya ya virusi vya Corona, hali iliyorekodiwa katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Kuanzia Jumatano, sheria ya kutotoka nje itaanza kutumika katika mji mkuu wa Senegal, Dakar na viunga vyake, ambapo sehemu kubwa ya maambukizi yameripotiwa. Uvaaji wa barakoa itakuwa lazima na mikusanyiko mikubwa imepigwa marufuku.

Hatua hiyo inakuja miezi sita baada ya hali ya dharura ya kwanza kuondolewa kwa matumaini ya kufufua uchumi ulioathirika sana na vizuizi vya kiafya wakati wa wimbi la kwanza la janga hilo.

Tangu kuzuka kwa mgogoro wa kiafya, Senegal imeripoti visa 19,964 vya maambukizi na vifo 428.