JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

CAR: Ukosefu wa usalama wauweka matatani mchakato mzima wa uchaguzi

Wanasiasa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
Wanasiasa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati FLORENT VERGNES / AFP

Wabunge 21 kati ya 140 ndio walioibuka washindi katika duru ya kwanza ya uchaguzi, kulingana na matokeo ya awali ya uchaguzi.

Matangazo ya kibiashara

Duru ya pili itafanyika katika maeneo 61 ya nchi hiyo. Lakini, ukosefu wa usalama uliwazuia raia wengi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, na kuibua maswali mengi juu ya hatua inayofuata katika mchakato huo.

Baada ya uchaguzi, maeneo 58 hayakuweza kupiga kura kwa sababu ya ukosefu wa usalama. Baadhi ya waangalizi wanahoji kuhusu uchaguzi ujao katika maeneo haya.

Jean-Symphorien Mapenzi, Naibu Spika wa Bunge, ana matumaini juu ya muda uliopangwa kutekelezwa.

“Katika ngazi ya Bunge, hakuna cha kuwa na wasiwasi. Mradi muhula wetu utaendelea hadi Mei 2, kwa hivyo tunasubiri hadi duru ya pili imalizike na maeneo ambayo hayakuweza kupiga kura yawe na uchaguzi wao kabla ya kujadili suala lolote, " Jean-Symphorien Mapenzi amesema.

Hayo yanajiri wakati wagombea urais kumi kati ya kumi na sita walisema mapema wiki hii katika taarifa kwamba hawatambui matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais wa Desemba 27, 2020 na wanataka uchaguzi huo "kufutwa."

Siku ya Jumatatu wiki hii, Tume ya Uchaguzi (ANE) ilimtangaza rais anayemaliza muda wake Faustin-Archange Touadéra kushinda uchaguzi huo katika duru ya kwanza kwa zaidi ya 53% ya kura zilizopigwa.

Matokeo ambayo yalihusu nusu tu ya wapiga kura. Nusu nyingine haikuweza kupiga kura kutokana na mashambulio ya waasi yanayoendelea nchini.

Wagombea hao kumi wamebaini kwamba uchaguzi wa urais wa Desemba 27 ni "pingamizi kubwa kwa demokrasia", na wamekiri kuwa hawatokubali 'ushindi na uhalali' wa rais aliyetangazwa mshindi na kuomba uchaguzi huo ufutwe.