DRC

Muungano Mtakatifu DRC: Lambert Mende kujiunga na kambi ya Tshisekedi

Rais wa DRC Felix Tshisekedi akiwa ziarani mjini Goma mwaka 2019
Rais wa DRC Felix Tshisekedi akiwa ziarani mjini Goma mwaka 2019 ALEXIS HUGUET / AFP

Wengi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanajiuliza maswali mengi kuhusu wanasiasa wa nchi hiyo ambao hawana msimamo katika siasa zao.

Matangazo ya kibiashara

Masuali hayo yamekuja baada ya Waziri wa Habari na msemaji wa serikali katika utawala wa joseph Kabila na mshirika wa rais huyo wa zamani anajiandaa kujiunga na kambi ya rais Tshisekedi, na kujitenga na kambi ya kiongozi wake Kabila.

Januari 6, Lambert Mende, waziri wa zamani wa Joseph Kabila alikutana kwa mazungumzo na Felix Tshisekedi na kuzungumzia kuhusu kujiunga kwake katika muungano huo wa kisiasa wa rais wa jamhuri.

Kulingana na gazeti la Jeune Afrique, wawaili hao walikutana Januari 6 kwa muda wa saa moja na kuafikiana katika masuali mbalimbali.

Akiambatana na mmoja wa washirika wake wa karibu, Thierry Monsenepwo, kada wa muungano wake cha kisiasa wa CCU na washirika wake kadhaa, Mende alikamilisha mchakato wa kujiunga katika miuungano mpya wa kisiasa ulioanzishwa na rais Felix-Antoine Tshisekedi (Muungano Mtakatifu) ambao unakuja kukabiliana na ushawishi wa Joseph Kabila.