ETHIOPIA

Jeshi la Ethiopia lamuua afisa wa juu wa kikosi cha TPLF jimboni Tigray

Jeshi la Ethiopia likiendelea na operesheni zake katika jimbo la Tigray
Jeshi la Ethiopia likiendelea na operesheni zake katika jimbo la Tigray REUTERS/Tiksa Negeri/File Photo

Jeshi la Ethiopia linasema limemuua afisa wa juu wa kikosi cha jimbo la Tigray People’s Liberation Front (TPLF) baada ya kufanya operesheni katika jimbo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Ethiopia linasema  miongoni mwa maafisa wengine waliouawa ni pamoja na Sekoture Getachew msemaji wa kikosi hicho cha TPLF na aliyekuwa mkuu wao wa kitengo cha fedha Daniel Assefa

Zeray Asgedom, aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini humo ameuawa pia katika operesheni hiyo.

Taarifa ya jeshi la Ethiopia, imesema kuwa maafisa tisa wa jeshi hilo la Tigray pia wamekamatwa katika opereheni hiyo.

Mwezi Novemba mwaka 2020, wakati jeshi la Ethiopia lilioanza opereheni katika jimbo hilo, serikali jijini Addis Ababa ilitangaza kuakamatwa viongozi wakuu wa jimbo hilo wapatao sitini.

Jeshi la Ethiopia limeendeleza operesheni katika jimbo hilo licha ya kudai kuwa, ilifanikiwa kulidhibiti.