COTE DVOIRE

Côte d’Ivoire yakabiliwa na ongezeko la visa vya maambukizi

Kirusi cha Corona
Kirusi cha Corona NEXU Science Communication | Reuters

 Côte d’Ivoire ina visa 23,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona vifo vivyozidi 140 vimerekodiwa tangu kuzuka kwa janga hilo nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo takwimu mbaya za siku za hivi karibuni zinatia wasiwasi. Walakini, bado ni mapema sana kuzungumzia juu ya mlipuko wa pili wa virusi hivyo nchini Côte d’Ivoire.

Pamoja na zaidi ya visa 800 kwa wiki moja (pamoja na visa 210 zilizorekodiwa Alhamisi pekee), ongezeko la idadi ya visa vilivyothibitishwa tangu mwishoni mwa mwezi Desemba linaendelea.

Kiwango cha watu walioambukizwa virusi vya Corona, ambacho kimebaki chini ya 5% katika miezi ya hivi karibuni, ikiwa ni kizingiti kinachowezesha kuzingatia kwamba janga hilo limedhibitiwa, imekuwa ikiongezeka kwa kasi katika siku chache zilizopita.