CAMEROON

Kumi na wawili waangamia katika shambulio la bomu kaskazini mashariki mwa Cameroon

Magaidi wa Boko Haram
Magaidi wa Boko Haram AFP

Shambulio ambalo serikali ya Cameroon inahusisha kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Boko Haram limeuawa watu wasiozidi 12 na kujeruhi wengine wengi, kulingana na vyanzo kutoka Cameroon.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo hivyo kundi la Boko Haram lilifanya uvamizi katika mji wa Mozogo siku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa wiki hii.

Kundi lenye silaha liliingia katika eneo hili karibu saa 12:30 Asubuhi. Walianza kwa kuweka mabomu kwenye barabara zinazoingia katika kijiji cha Mozogo.

Waliendesha shambulio la kujitoa muhanga, imesema taarifa kutoka wizara ya mawasiliano, kabla ya kufyatua risasi kwa wakaazi wa mji huo.

Yaoundé imelihusisha kundi la Boko Haram kwa shambulio hilo, ambalo inadaiwa kuwa lilisababisha vifo vya watu wasiopungua kumi na wawili, wakiwemo raia kumi na mmoja na mmoja wa washambuliaji aliyejilipuwa kwa kujitoa muhanga.

Watu wengine wawili waliojeruhiwa, walipelekwa hospitalini, serikali imesema katika taarifa.

Mapema jana Ijumaa, mkuu wa jadi wa mji wa Mozogo na afisa wa polisi waliliambia shirika la habari la AFP kwamba raia 13 waliuawa na mshambuliaji wa kujitoa muhanga, ikiwa ni pamoja na watoto 8.