CONGO-BRAZZAVILLE

Rais Denis Sassou Nguesso kupeperusha bendera ya chama chake

Rais wa Congo Brazaville, Denis Sassou-Nguesso.
Rais wa Congo Brazaville, Denis Sassou-Nguesso. EVGENIA NOVOZHENINA / POOL / AFP

Rais wa Congo Denis Sassou Nguesso, 77, ameteuliwa rasmi na chama chake cha PCT, kuwania katika uchaguzi wa urais kwa tiketi ya chama hicho.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi nchini congo umepangwa kufanyika mwezi Machi 2021, lakini upinzani umeendelea kukishtumu chama tawala na serikali kuminya demokrasia nchini humo.

Chama cha PCT kimemumba kiongozi wake kukubali uteuzi huo. PCT kiko madarakani kwa miaka 46 sasa.

Mgombea wa chama cha PCT atachuana katika uchaguzi ho na Mathias Dzon, Waziri wake wa zamani wa Fedha kati ya mwaka 1997 na 2002, na Guy-Brice Parfait Kolélas aliyechukuwa nafasi ya pili katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2016.