MALI

Wanajeshi sita wa Barkhane wajeruhiwa nchini Mali katika shambulizi la bomu

Opereseheni ya kijeshi nchini Mali
Opereseheni ya kijeshi nchini Mali defense.gouv.fr/operations

Wanajeshi sita wa kikosi cha Barkhane nchini Mali wamejeruhiwa katika shambulizi la kujitoa muhanga aliyetumia gari lililokuwa limetegwa bomu.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo ni la tatu dhidi ya wanajeshi wa Ufaransa tangu mwishoni mwa mwezi wa Desemba, makao makuu ya jeshi la Ufaransa yamebaini.

Shambulio hilo lilitokea Ijumaa asubuhi, katika eneo linalojulikana kama mipaka mitatu (Mali, Niger, Burkina Faso), wakati gari lililokuwa limetegwa bomu lilipoelekezwa kwa kasi kubwa kuelekea upande wa nyuma wa msafara wanajeshi wa kikosi cha Barkhane wanaoshirikiana katika opereshini mbalimbali na askari wa Mali, kulingana na taarifa.

Wanajeshi sita wa Ufaransa walisafirishwa kwenda hospitali ya Gao lakini wanaendelea vizuri, jeshi la Ufaransa limeongeza.