AFRIKA KUSINI-COVID 19

Masharti zaidi yatangazwa nchini Afrika Kusini kudhibiti janga la Covid 19

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Jerome Delay / POOL / AFP

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ametangaza masharti zaidi yanayolenga nchi hiyo yenya mamabukizi makubwa ya virusi vya corona barani Afrika, kudhibiti janga hilo.

Matangazo ya kibiashara

Uzwaji wa pombe umepigwa marufuku, lakini pia safari za ndnai ya nchi hiyo zimesitishwa hadi katikati ya mwezi Februari.

Safari za malori yanayosafirisha mizigo ndani na nje ya nchi hiyo zitaendelea, lakini sio kila mtu atakayeruhiswa kuingia katika taifa hilo, isipokuwa wanafunzi na watu wanaokuja kutafuta huduma ya afya.

Nchi  hiyo imerekodi maambukizi zaidia ya Milioni Moja na Laki mbili na vifo zaidi ya Elfu 30.

Mwishoni mwa mwaka 2020, maambukizi ya Corona yalifikia zaidi ya Milioni moja katika taifa hilo.