TUNISIA

Tunisia yaadhimisha miaka 10 tangu kuangushwa kwa utawala wa Zine el Abidine Ben Ali

Kiongozi wa zamani wa Tunisia Zine El Abidine Ben Ali wakati wa uhai wake
Kiongozi wa zamani wa Tunisia Zine El Abidine Ben Ali wakati wa uhai wake Handout / AFP

Tunisia wiki hii inaadhimisha miaka 10 tangu kuangushwa kwa utawala wa muda mrefu wa Zine el Abidine Ben Ali, baada ya maandamano ya raia kutaka mageuzi ya kisiasa na kiuchumi.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa zamani wa Tunisia Zine el Abidine Ben Ali ambaye aliiaga dunia mwezi septemba mwaka 2019 akiwa uhamishoni huko Saudia Arabia alikokimbilia baada ya kutimuliwa madarakani kufuatia maandamano ya umma, hatua ambayo ilisababisha wimbi la maandamano katika ulimwengu wa kiarabu.

Ben Ali alioongoza nchi hiyo kwa miaka 23 na alipongezwa kwa kuidhinisha utulivu na ufanisi kwa kiasi fulani wa kiuchumi.

Hata hivyo kiongozi huyo alishutumiwa pakubwa kwa kukandamiza uhuru wa kisiasa na kueneza ufisadi kwa kiwango cha juu nchini humo.

Kipindi anaingia uongozini mwaka1987, aliahidi mageuzi, demokrasia , haki kwa wanawake na elimu, lakini wananchi wa Tunisia walionesha kuchoshwa na utawala wake baada ya kuwepo madarakani kwa muda mrefu..

Januari 14,mwaka huu Watunisia watakumbuka siku ya walipomtimua kiongozi huyo, huku wengi wakisikitikia kitendo hicho na baadhi wakithibitisha kuanguka kwa uchumi wa taifa hilo hata baada ya kiongpozi huyo za zamani kuangushwa.