NIGERIA

Wanajeshi 13 wauawa Kaskazini Mashariki mwa Nigeria

Gari la kundi la kigaidi la ISWAP Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Gari la kundi la kigaidi la ISWAP Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. AUDU MARTE / AFP

Wanajeshi kumi na watu wa Nigeria, wameuawa baada ya kushambuliwa na wanajihadi wa Islamic State ISWAP, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya jeshi nchini humo imethibitisha kuuawa kwa wanajeshi hao, baada ya msafara wao kushambuliwa na silaha nzito katika kijiji cga Gazagana katika jimbo la Yobe.

Wanajeshi wengine ambao idadi yao haijatajwa, walijeruhiwa katika shambulizi hilo lililowamlenga maafisa hao wa usalama waliolkuwa njiani kurejea katika kambi yao huko Buni Yadi baada ya opereheni yao.

Hata hivyo, jeshi la Nigeria nalo linasema kuwa lilifanikiwa kuwauwa wanajihadi kadhaa wa kundi hilo la ISWAP.

Tangu mwaka 2009, jeshi la Nigeria limekuwa likipambana na wanajihadi Kaskazini mwa nch hiyo, eneo ambalo lina magaidi wa Boko Haram, ambao wamesababisha vifo vya watu zaidi ya Elfu 36 na wengine zaidi ya Milioni Mbili kuyakimbia makwao.