AFRIKA

Afrika kuagiza dozi Milioni 300 kupambana na janga la Corona

Chanjo aina ya Moderna
Chanjo aina ya Moderna Photo AP / Hans Pennink

Umoja wa Afrika umefanikiwa kuagiza dozi Milioni 300 ya chanjo ya virusi vya corona kwa  mujinu wa kituo cha kudhibiti magonjwa, CDC.

Matangazo ya kibiashara

Mshauri wa kituo hicho Nicaise Ndembi, ameliambia Shirika la Habari la Uingereza, Associated Press kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, atatangaza siku ya Jumatano.

Kupatikana kwa chanjo hiyo itaanza kutoa matumaini kwa nchi za Afrika katika kudhibiti virusi hivyo ambavyo vimewaambukiza watu 3,085,009 na vifo 73,504.

Bara la Afrika lenye watu Bilioni 1 na Laki mbili, limefanya mpango wa kupata chanjo hiyo kupitia Shirika la Covax, ambalo linaundwa na Shirika la afya duniani WHO, Umoja wa Ulaya na Ufaransa.

Mbali na Umoja wa Afrika, nchi moja moja ya Afrika inafanya mpango wa kupata chanjo.

Afrika Kusini wiki iliyopita, ilitangaza kuwa itapokea dozi Milioni mpja ya chanjo kutoka kituo cha Serum nchini India mwezi Januari na awamu ya pili ya kupata dozi  500,000 zitakuja mwezi Februari.