MALAWI-COVID 19

Rais Chakwera atangaza hali ya dharura kukabili janga la Corona

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera AMOS GUMULIRA / AFP

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ametangaza hali ya hatari kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona nchini humo ambayo yamefikia zaidia ya Elfu tisa na vifo zaidi ya mia mbili.

Matangazo ya kibiashara

Mbali na ongezeko hilo, hatua hii inakuja baada ya Mawaziri wake wawili kufariki dunia kutokana na virusi hivyo.

“Kila mmoja wetu lazima aijali afya ya mwingine   na kila mmoja wetu lazima avae barakoa  hadharani  lazima aoshe mikono kabla na baada ya shughuli yoyote,”.

“Lazima tuweke  umbali  na wengine ili kuepuka maambukizi,na tuondoke kwenye maeneo yakiyojazana watu maana hakuna mmoja wetu yupo salama  kwa hiyo inamaanisha kila mmoja wetu lazima awajibike, amesema.

Maombolezo ya kitaufa ya siku tatu yametangzwa nchini humo kuwakumbuka watu waliopoteza maisha.