JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wajaribu kuvamia jiji kuu Bangui

Jeshi la Umoja wa Mataifa Minusca, jijini Bangui
Jeshi la Umoja wa Mataifa Minusca, jijini Bangui AFP PHOTO / EDOUARD DROPSY

Waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wamejaribu kuvamia jiji kuu Bangui, baada ya kutekeleza mashambulizi mawili, lakini wamerudishwa nyuma.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa usalama wa ndani Henri Wanzet Linguissara na maafisa wa jeshi la Umoja wa Mataifa,wamethibitisha kutokea kwa jaribio hilo.

Msemaji wa jeshi la Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCA, Abdoulaziz Fall, amesema makabiliano yanaendelea kuwazuia waasi hao.

Tukio hili linakuja, wakati huu muungano wa waasi unaongozwa na rais wa zamani Francois Bozize, ukishtumiwa kuwa na mpango wa kutaka kuipundua serikali.

Mwezi Desemba mwaka 2020, uchaguzi uliofanyika nchini humo na rais Faustin-Archange Touadéra kuchaguliwa tena.